top of page
Praying_edited_edited.jpg

"Nifuate kama mimi nimfuate Kristo"

( 1 Wakorintho 11:1 )

DHAMIRA YETU

 “ Kufanya tu yale yampendezayo Mungu.” ( Yohana 8:28-29 )

“Tazama, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu. 

Na Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula;

Hata Mtume wa ahadi, mnaye mfurahia.

Tazama, anakuja, asema BWANA wa majeshi!" 

( Malaki 3:1 )

 

Kugusa upendo wa Mungu, tunatoa jukwaa na mazingira ambapo mtu yeyote anaweza kupokea na kufanya mipango ya Mungu (Baraka) kwa maisha yake kwa wingi zaidi!

Kila mjumbe katika misheni ya UAMSHO anaendesha hivi,

  • Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa kila kiumbe hai ( Marko 16:15-18 )

  • Kuhubiri na Kufundisha Neno la Mungu safi na lisiloghoshiwa kwa kila Mtu, Mhudumu, Familia, Kanisa na Mataifa. ( Yohana 17:17 )

  • Kuwarejesha na Kuwarudisha watu kwa Mungu wa Kweli na Aliye Hai; Roho Mtakatifu akihuisha maisha yenyewe na upendo wa Mungu ndani yao.

  • Kurejesha Neno la Mungu kama msingi na kiwango cha Kristo kwa maisha ya Kikristo … “ili imani ya wanadamu isisimame katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za MUNGU.”( 1 Wakorintho 2:2-5 )

Kuhuisha na Kurejesha Kanisa kwa matendo ya: 

  • Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa na hekima...( Mithali 1:7, Zaburi 111:10 )

  • Ibada ya Kweli…. Kwa maana Mungu anawatafuta watu kama hao wamwabudu( Yohana 4:21-24 )

  • Utakatifu wa Kweli na Maisha Matakatifu…. Kufuatana na Amani na watu wote na Utakatifu, ambao hapana MTU atakayemwona Bwana asipokuwa nao! (Waebrania 12:14, 1 Petro 1:16)

 

Kuhuisha na Kurejesha Kanisa kwa wito wa huduma ya kweli ya Uinjilisti na Uanafunzi ( Mathayo 28:18-20 )

bottom of page